ASKOFU KIMANGICH:Jitumeni kwa uinjilishaji

Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa Misa ya kwanza ya kihistoria katika eneo la maombi ya Kabiyet dekania ya Kaiboi.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic kimengich akiadhimisha daraja la upadre kwa nashemasi tisa ametoa wito kwa mashemasi hao kujisadaka bila kujibakjsha ili kuishi wito wao na kuwa mfano Bora kwa wakristu.

Askofu Kimengich akiwataka kuwa watu wa Sala siku zote ili awaongoze katika utendakazi wao akiwataka kadhalika kushirikiana na na padre wengine kwa akili ya maelekezi.

Alitoa wito kwa mapadre hao wapya kuwa wanyenyekevu katika wito wao akiwataka kuwa tayari siku zote kuwasamehe wale watakaowakwaza katika utendakazi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *