GAVANA CHELILIM :Acheni ukabila

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amewataka Wenyeji kuepuka maswala ya ukabila kwa faida ya mshikamano kwa kaunti hii.

Akiongea katika kanisa la kianglikana la St.Mathews mjini Eldoret, wakati wa hafla ya kina mama, Gavana Chelilim alisema kwamba ukabila ni jambo lililopitwa na wakati, akisema kuwa  wakaazi wanastahili kuishi Kwa pamoja Kwa kutangamana na kukumbatiana ikiwa ni dhihirisha ya ujirani mwema.

Alisema kwamba mji wa Eldoret una wàtu kutoka jamii mbalimbali, akitoa wito kwao kuishi Kwa amani na kusaidia ukuaji wa uchumi wa kaunti kupitia biashara zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *