ASKOFU OKEMWA:Hudumieni wakenya acheni siasa

Askofu wa jimbo katoliki la Kisii askofu Joseph Mairura Okemwa, aLItoa wito kwa viongozi kutoka mirengo yote ya kisiasa kuzika tofauti zao na badala yake kuwahudumia wakenya.

Askofu Mairura aliwataka viongozi nchini kuangazia maslahi ya wananchi na kuangazia changamoto ambazo kwa sasa zinakumba wakenya, zikiwemo baa la njaa ukosefu wa maji na ukame nchini.

Aliwataka viongozi hao kutoegemea mirengo ya kisiasa akisema kuwa wakati wa kampeni umekwisha, ikiwa sasa ni wakati wa kushirikiana kwa pamoja kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *