ARCHBISHOP KAMBANDA:Upendo udumu

Wito umetolewa kwa wakristu kuonyesha upendo wao kwa wenzao kwani hili linaonyesha kwamba wao ni wakristu watimilifu.

Kwa mujibu wa askofu mkuu wa Kigali Rwanda Antonie Cardinal Kambanda akiongea katika uwanja wa Kinoru Kaunti ya Meru  wakati wa hafla ya kumtawaza mtawa wa shirika la watawa wa Mt.Yosefu Benedetto Cottolengo alisema upendo ambao mtawa Carola alikuwa nayo alipokuwa akiendelea na shughuli ya uinjilishaji unadhihirisha kwamba bila upendo kupiga hatua katika maisha ni nadra sana kwa mkristu ambaye ana ndoto ya kuuridhi ufalme wa mbingu.

Kadhalika aliwashauri wakristu kuwasaidia wasiojiweza katika jamii na kuwaombea wote ambao hawajajaliwa mema maishani ili waweze kupata maisha bora hapo baadae.

Mtawa Maria Carola alizaliwa mwaka wa 1877 katika eneo la Cittadella nchini Italia na kuingia nchini kama mishonari mnamo mwaka wa 1905 katika kanisa la Tigania dyosisi ya Meru na atakuwa mtawa wa pili katika historia ya Kenya kutawazwa mtakatifu baada ya kutawaza kwake mtawa Irene ‘Nyaatha’ Stefani aliyetawazwa mwaka wa  2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *