Askofu wa Jimbo katoliki ya Lodwar John Mbinda amewataka wakenya kuchukua hatua ya kujua hali yao ya afya ndipo waweze kuwa salama dhidi ya unyanyapaa unatokana na maambukizi ya magonjwa sugu.
Akiongea baada ya kuongoza ibada ya Misa katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali askofu Mbinda amewaomba wakenya kufahamu kwamba afya nzuri itawasaidia kuyatekeleza majukumu yao ipasavyo na kujiinua kimaishani.
Aidha,askofu aliitaka wizara ya afya nchini kuhakikisha kwamba wakenya wamepata kuhamasika ipasavyo kuhusiana na maswala ya afya na umuhimu wa kujua usalama wa afya yao kila wakati.
Wakati huo aliwaomba wahisani kujitokeza na kuwapa msaada wa chakula wakenya ambao wameathirika na baa la njaa nchini akiwasihi kuonyesha Upendo wao bila mapendeleo yoyote.