WAKULIMA WA UASIN GISHU WAHIMIZWA KUPANDA MIMEA MBADALA

Waziri wa kilimo katika kaunti ya Uasin Gishu Samwel Yego aliwaomba wakulima kuona kwamba wamejihusisha kwa kilimo biashara.


Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,Yego anasema ni muda sasa wakulima wanastahili kukoma kutegemea tu kilimo cha mahindi na wanalo uwezo wa kushiriki kilimo cha mimea tofauti ikiwemo kilimo cha parachichi ,macademia na hata ya kahawa.


Yego alidokeza kwamba kwa miaka mingi sasa wakulima walikuwa wakijihusisha na uzalishaji wa mahindi na nafaka na yastahili waweze kufungua macho na kukuza mimea hiyo akidai soko iko tayari akidokeza kuwa kupitia hili pia wanaweza wakajikimu kimaisha na kujipatia pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *