Baba mtakatifu Francisko amemteua padre Hieronimus Joya, kama askofu wa jimbo katoliki la Maralal.
tangazo hili limetolewa hii leo saa sita mchana na Baba mtakatifu Francisko kule Vatican na kutumwa kwa ,mwakilishi wa Baba mtakatifu nchini na Sudan Kusini Mwadhama Mathews Herbatus Van Megen na kutumwa kwa baraza la maaskofu wakatoliki nchini KCCB.
uteuzi huu unajiri baada ya kustaafu kwa askofu wa jimbo hilo la Maralal askofu Virjilio Pante aliyefikisha umri wa kustaafu kutokana na sheria za kanisa katoliki.