BISHOP:Acheni malumbano

Wito umetolewa kwa wanasiasa hasa kwa rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kutatua tofauti zao bila ya kulumbana hadharani.

Kwa mujibu wa askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich,malumbano hayo na kutoleana cheche za maneno baina ya rais na naibu wake inasikitisha mno ikizingatiwa kuwa wao ndio viongozi ambao wakenya wanastahili kuwaiga na iwapo wataendelea kukabiliana hadharini basi wakenya wanaweza wakakosa mwelekeo kwa uongozi nchini au hata kukosa imani na wanasiasa.

Hata hivyo,askofu aliwataka viongozi nchini kuwa mfano mwema kwa wananchi na kuwafanyia maendeleo wakaazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *