Askofu Wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich aliwarai wazazi kuwakaribia wanao msimu huu wa likizo fupi wasije wakajiingiza kwenye maswala yasiyofaa.
Akiongea afisini mwake mjini Eldoret askofu alibaini kwamba wazazi wengi wamesahau majukumu yao na hili limechangia upotovu wa maadili kwa wanafunzi hao.
Vilevile askofu aliwashauri viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele pia kuwaombea watoto hao wasije wakapatikana kwenye maswala yasiyostahili ikiwemo matumizi ya mihadarati.
