Gavana wa kaunti ya Elgeyo-Marakwet Alex Tolgos amewataka wanasiasa kuendesha kampeni zao kwa njia ya amani na kuepukana na uchochezi taifa linapojiandaa kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9 mwaka huu.
Akiongea katika parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Iten katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet,alidokeza kuwa ni wakati sasa wakenya waruhusie kuendeleza demokrasia yao ya kuwachagua viongozi wanaowaenzi bila ya kushurutishwa kwa hili akisema sharti kila mkenya kuwajibikia matamshi yake.
Wakati huo,Tolgos akiipigia debe muungano wa Azimio la Umoja One Kenya linaloongozwa na mpeperushaji bendera la urais Raila Odinga akieleza kuwa uongozi wa muungano huo wa kisiasa itakapo twaa ushindi na kuingia madarakani maswala za kimsingi ikiwemo kuwaajiri walimu ambalo ametaja limekua donda ndugu kuweza kutekelezwa kwani anadai anaamini mahitaji na matakwa ya wakenya ya kuajiriwa kwa walimu wengi itaafikiwa.