Padre mkuu wa jimbo hili la Eldoret William Kosgei amewashauri wakristu kuwa tayari kulieneza injili yake Yesu Kristu kila wakati kwa kusimama imara katika huyo kristu.
Katika homilia yake Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Iten alisisitiza kuwa japo wapo maaskofu,mapdre,makasisi,wahubiri na viongozi wengi wa kidini katika ulimwengu huu,haimainishi kuitikia mwito wa kulieneza injili hiyo kwa mkristu imetosha bali wanastahili kujukumika katika kukuza imani yao na kristu kila mara.
Vilevile padre Kosgei aliwatahadharisha dhidi ya kupotoshwa na matamanio ya ulimwengu na Kuwashauri kujihusisha na yale yatakayo waongoza kila wakati kuwa karibu na Mungu kwani anasema hata kama watayapitia changamoto maishani wataweza kuyashinda kupitia kristu mwezeshaji wa yote.