Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret amezindua rasmi mchakato wa kushirikisha ruwaza ya Baba mtakatifu Francisko wa kupanda miti kama njia moja ya kuhifadhi mazingira.
hii inajiri baada ya Baba Mtakatifu Francisko kutangaza kuzinduliwa kwa Jukwaa la Kazi la Laudato si, “Laudato si Plaform of Action, LSAP”, safari shirikishi ya miaka saba, kama sehemu ya mchakato wa kujizatiti kikamilifu katika maendeleo na ekolojia fungamani.
askofu kimengich amehaidi kushirikiana na parokia mbalimbali jimboni pamoja na shule ili kuwepo na mtindo wa kupanda miche katika maeneo tofauti jimboni ili kufanikisha mchakato huu wa laudato si.
ikumbukwe kuwa baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu linaendelea na mchakato wa kuchapisha Kitabu cha mashuhuda wa “Laudato si” utunzaji bora wa mazingira unaobubujika kutoka katika sakafu ya maisha ya watu, mazingira pamoja na maeneo yao ya kijamii.
