Baraza la wahubiri na maimam (CIPK) Kanda la Kaskazini mwa bonde la ufa limeelezea hofu yao kuhusu idadi kubwa ya wagombea wa kiti cha urais likisema huenda limechangiwa na kutokuwepo Kwa Imani Kwa vyama vya kisiasa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza hilo kanda la North Rift Sheikh Abubakar Bini amesema hatua hiyo ni hatari kwa demokrasia na inaonyesha ukosefu wa maadili katika vyama vya kisiasa.
Akizungumza mjini Eldoret Bini amesema idadi ya wagombea urais huru ya zaidi ya 30 ni idadi kubwa zaidi akisema huenda walinyimwa nafasi kwenye vyama vya kisiasa kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa nchini.
Ametoa wito wa kubiniwa kwa sheria ambayo itachangia kuboresha demokrasia katika vyama vikuu vya kisiasa ili kulinda wafuasi wa vyama hivyo na wagombeaji viti mbalimbali vyamani humo.