ASKOFU KORIR AKUMBUKWA

Wito umetolewa kwa waumini wa jimbo hili katoliki la Eldoret kuwa na upendo na amani miongoni mwao jimbo linapoadhimisha kumbukumbu ya mwendazake askofu Cornelius Kipng’eno Arap Korir.

Akiongoza misa ya kumbukumbu ya askofu Cornelius Korir aliyeaga dunia miaka minne iliyopita, askofu wa jimbo hili Dominic Kimengicha amenkumbuka mwendazake kama mtu aliyelitumikia jimbo hili kwa kujisadaka bila kujibakisha kwa kupatanisha na kuleta amani miongoni mwa jamii ambazo kila mara zimekuwa zikishuhudia machafuko.

Katika misa iliyowaleta pamoja kikundi cha wanaume wakatoliki jimboni CMA askofu Kimengich amewataka wanaume wote kuchukua jukumu la kulinda familia yao na jamii kwa ujumla kwa mapendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *