Serikali yatakiwa kuekeza zaidi katika kilimo cha mahindi

Wakulima kutoka kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa sasa wanashinikiza serikali ya kitaifa kupitia wizara ya kilimo, kuweka mikakati kabambe ya kununua mahindi takriban magunia milioni mbili ya wakulima kutoka eneo hilo ili kuinua mapato yao.

Wakizungumza mjini Eldoret wakiongozwa na mwenyekiti wao Kipkorir Menjo, wakulima hao wameishtumu serikali kwa kukosa kuekeza rasilimali za kutosha katika sekta ya kilimo hasa kilimo cha mahindi ikizingatiwa kuwa ndicho chakula cha wengi.

Menjo amesema wakulima wengi wamevunjika moyo katika ukuzaji wa zao la mahindi kutokana na serikali kukosa kuangazia maslahi yao. Anaitaka serikali kuongeza bei ya kununua mahindi hadi Sh.3, 000 kwa kila gunia la kilo tisini ili kuwaoa motisha wakulima kuendeleza kilimo cha zao hilo.

Kwa upande wake mbunge wa Moiben Silas Tiren ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa, ameitaka serikali kupunguza bei ya pembejeo na vifaa vingine vya kilimo ili kuinua kiwango cha uzalishaji wa chakula nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *