Kaunti ya Uasin Gishu Yapongezwa Kuhusu Miradi

Msimamizi wa bajeti nchini Margaret Nyakang’o amesifia serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kutokana na utekelezwaji wa miradi ya maendeleo, kadhalika kuimarika kwa kiwango cha ushuru.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika kaunti hiyo, Bi Nyakang’o aidha, amepongeza kaunti ya Uasin Gishu kwa kupitisha kiwango chake cha ushuru cha shilingi milioni 991 katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020 hadi shilingi bilioni 1.11katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

Amesema kuwa kaunti ya Uasin Gishu ni miongoni mwa kaunti chache nchini ambazo zimefanya vyema katika ukusanyaji ushuru akiongeza kuwa hali hiyo inaashiria kuwa kaunti hiyo ina uwezo wa kufanya vyema hata zaidi katika miaka ijayo ya kifedha.

Wakati uo huo msimamizi wa bajeti amepongeza serikali ya gavana Jackson Mandago kwa kulipa madeni kwa wakati unaofaa na pia kuzingatia usawa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wadi zote 30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *