CWA-Eldoret wamtembelea Baba Askofu

Askofu wa jimbo Katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewahimiza kina mama kudumu katika sala ili kuimarisha imani yao.

Akiongoza Misa takatifu kwa ajili ya kikundi cha Wamama Wakatoliki (CWA) Jimbo La Eldoret katika uwanja wa upadirisho hapa mjini, askofu Kimengich amesema nguzo muhimu katika maisha ya mkristu ni imani na kusali kila wakati ili kumpendeza Mungu.

Wakati uo huo askofu Kimengich amewapongeza kina mama kwa mchango wao wa kueneza injili na kujenga imani katika familia, jumuiya na jamii nzima.

Aidha askofu amewasihi kina mama kuishi vema wito wao wa kifamilia kwa kudumisha upendo na uvumilivu kwa mujibu wa mafundisho ya kanisa ili pia kanisa liweze kudumu.

Amewataka kina mama kuiga mfano wa Mama Bikira Maria kwa kuwa wapole na wenye imani isiyo na mipaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *