Kiswahili Kitukuzwe Bungeni

BUNGE la Kitaifa linatarajiwa kupiga hatua muhimu katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kuendeshea shughuli zake kwa kuzindua kanuni za bunge zilizotafsiriwa kwa lugha hiyo, leo.

Hafla ya uzinduzi imepangiwa kuongozwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya Hotuba yake kuhusu Hali ya Taifa mbele ya kikao cha pamoja cha Bunge la Taifa na Seneti.

Itakuwa mara ya kwanza kwa wabunge kuanza kutumia kanuni ziliandikwa kwa Kiswahili japo baadhi yao wamekuwa wakichangia mijadala kwa lugha hii kwani ni mojawapo ya lugha rasmi bungeni, kulingana na kipengele cha 120 cha Katiba ya Kenya.

Karani wa Bunge la Kitaifa Michael Sialai alisema uzinduzi huo ni kilele cha shughuli ya utafisiri, na usanifishahi wa kanuni hizo, iliyoendeshwa na jopo kazi maalum kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

Jopokazi hilo lilisaidiana na maprofesa wa Kiswahili kutoka vyuo vikuu vya Kenya na wataalamu wa lugha hii kutoka Kenya na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA).

Mchakato wa kutafsiri kanuni za Seneta kwa Kiswahili pia umeanza na unatarajiwa kukamilika mapema mwaka ujao.

Afisa wa bunge ambaye ni mwanachama wa jopokazi lililooendesha kazi ya hiyo ya kwamba mradi huo ni sehemu mpango mpana wa asasi ya bunge kuandaa sajili rasmi ya bunge; lugha ya mahsusi itakuwa ikitumika na wabunge kuandaa hoja na miswada na kushiriki mijadala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *