walimu wote kote nchini wamepongezwa kwa kazi nzuri ambayo wanafanya katika kuimarisha sekta ya elimu
akiongea na kituo hiki padre raphael opondo kutoka idara ya elimu amepigia upatu siku hii ya kushrehekea walimu kote duniani kama yenye manufaa kwao kutoka na majukumu yao ya elimu
aliweza kuwashukuru wale ambao wamestaafu kutokana na matunda yao mazuri katika jamii huku akiwatia moyo walimu ambao wanaendelea kuhudumu kando na changamoto zinazowakumba
amewashauri walimu kuvumilia kwa kupeana elimu bora haswa wakati huu wa janga la corona kwa kukubali wito wowote na kupeana elimu inayohitajika