Afisa wa mauwaji ya barakoa afikishwa mahakamani

Afisa wa polisi aliyemfyatulia risasi na kumuua mshonaji wa viatu eneo la Lessos kaunti ya Nandi ameshtakiwa kwa mauaji katika mahakama mjini Eldoret.

Afisa huyo Sammy Onyango ambaye tayari amepigwa kalamu aliwasilishwa mbele ya Jaji Hellen Omondi kwa madai ya kumpiga risasi Lazarus Tirop.

Mahakama iliarifiwa kwamba Onyango alimuua Tirop Juni 25 alipojaribu kutatua mabishano yaliyozuka baada ya afisa huyo kumuitisha mhudumu wa bodaboda KSh 50 kwa kutovalia maski.

 Ripoti zilisema polisi huyo alifanyiwa uchunguzi wa kiakili na kupimwa dhidi ya COVID-19 kabla ya kufikishwa mahakamani.

Wakili wa Onyango Judy Muriuki aliiomba mahakama kumwachilia mshukiwa kwa dhamana na ombi hilo hilo litasikizwa Ijumaa, Julai 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *