Serikali ya kaunti ya busia kupitia idara ya afya imeeleza kusikitishwa na hatua ya wenyeji haswa katika eneo la airstrip mjini busia kupuuza masharti yaliyowekwa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona licha ya idadi ya waathiriwa kuongezeka kila kuchao.
Mkurungenzi wa afya katika serikali ya kaunti ya busia daktari Janerose Ambuchi amesema kwamba licha ya kuwepo kwa mikakati za kupambana na virusi vya corona baadhi ya wanachi wamepuuza maagizo na kuendelea kutangamana haswa madereva wa lori bila kujali hatari iliopo.