Huduma ya polisi imemrejesha kazini afisa mmoja mkuu wa polisi John M’mbijiwe, aliyekuwa akihudumu katika ukanda huu wa bonde la ufa ambaye alisimamishwa kazi kwa ajili ya sakata ya polisi Waiganjo .
M’mbijiwe sasa ameteuliwa kuwa naibu inspekta jenerali.
Katika barua ya juni tarehe 9 , huduma ya polisi imekubali kufutilia mbali hatua yake ya kumsimamisha kazi polisi huyo .
M’mbijiwe alisimamishwa kazi na kushtakiwa pamoja na Joshua Waiganjo ambaye alishtumiwa kwa kujifanya kuwa afisa wa ngazi ya juu wa polisi tangu mwaka wa 2012
Waiganjo anadaiwa kusafirishwa kwa helikopta za polisi na hata alikuwa kisafiri kutumia magari ya serikali .
Alikuwa akiwaaadhibu polisi wa vyeo vya chini ,kuwahamisha wengine ,kuongoza oparesheni za polisi na hata kukagua gwaride za heshima akiwa na sare yenye nembo ya naibu inspekta wa polisi .
Hata hivyo mwezi mei mwaka huu mahakama ya Nakuru ilimwondolea mashtaka yote baada ya upande wa mashtaka kukosa kuwasilisha usahidi dhidi yake . M’mbijiwe pia aliondolewa lawama baada ya mahakama kusema ushahidi uliotolewa haukutosha kuendeleza kesi yake .