Wito umetolewa kwa serikali kuu kupitia wizara ya afya kupima watu wote wanaotangamana na madereva wa malori ya masafa marefu dhidi ya virusi vya corona.
Katika mahojiano na kituo kiimoja cha habari humu nchini, naibu gavana wa kaunti Uasingishu Daniel Chemno ameshangazwa na jinsi vipimo hivi vinaendeshwa huku wanaotangamana na madereva hao wakisahaulika bila ya kuzingatia hathari ya kusambaa wa virusi vya corona. ametaka wizara ya afya kuweka mikakati ya kutosha kuhakikisha ya kwamba katika kila kituo ambacho madereva hao husimama na kutangama kila mtu amepimwa na kuthibitishwa iwapo ameambukizwa au la.