Askofu Mkuu Mstaafu Ndingi Mwana Anzeki Aaga Dunia.

Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu Katoliki la Nairobi Emeritus Raphael Ndingi Mwana A’ Nzeki ameaga dunia.

Taarifa kuhusu kifo chake imetolewa rasmi kwa umma mapema hii leo na kadinali John Njue ambaye amewashauri waumini wa Kanisa Katoliki kuiombea familia ya mwendazake wakati huu mgumu wa maombolezo.

Mwendazake ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuugua kwa muda.Nzeki, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1931, eneo la Mwala kaunti ya Machakos,  alijiunga na Seminari ya Kiserian baada ya kukamilisha masomo yake ya msingi.

Alipewa daraja la upadri mwaka wa 1961 na JJ McCarthy. Alipata Uaskofu mwaka 1969 na kuhudumu katika wadhifa huo katika majimbo ya  Machakos na Nakuru kabla ya kuteuliwa Kama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi mwaka wa 1996

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *