Chuo Kikuu cha Nairobi, bewa kuu, huenda kikafungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi hapo jana jioni kuzua fujo na kuteketeza bweni wakilalamikia kuuawa kwa mwenzao kwa njia tata.
Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo, aliyetambuliwa kama Kyte Ondeng, alishambuliwa na walinzi wanaolinda mabweni Jumatano wiki jana.
Samuel Ayoma ambaye ni kiongozi wanafunzi alisema kwamba marehemu alishambuliwa na walinzi hao ambao baadaye walimtelekeza katika uwanja wa Central Park, hatua chache kutoka majengo ya chuo hicho.