Buriani Kwa watoto wa mkasa Shule ya Msingi kakamega

Gavana wa kaunti ya kakamega Wycliffe Oparanya amewaongoza  viongozi pamoja na wakazi katika ibada ya mazishi ya wanafunzi 13 waliongamia  katika mkasa wa mkanyagano katika shule ya msingi ya kakamega

Akijumuika pamoja na magavana wengine, amewafariji familia  zilizopoteza wapendwa wao wakati huu mgumu akiwaomba wakubali msiba uliowapata na kuwa serikali itahakikisha kuwa wapendwa hao wamezikwa kwa heshima.

hata hivyo baadhi ya wazazi wa walioangamia  wamedai kutohusishwa kwenye maandalizi hayo kwa kutengwa na kuharakishwa kwa ibada ya mazishi sawa na fedha kutengwa kwa shughuli hiyo.

vilevile wametaka kamati ya matanga hayo kusitisha mipangao ya mazishi hadi watakapohusishwa na hata kupewa pesa za kugharania mazishi hayo la sivyo wenyewe watajisimamia.

Ni ibada inayojiri baada ya mwanafunzi mmoja aliyeangamia kwenye mkasa huo kuzikwa sambambamba na dini ya kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *