Maafisa Wakuu Waachishwa kazi Tenwek

Maafisa wakuu wanne wakiwemo wakurugenzi wa idara mbalimbali  katika hospitali ya Tenwek kaunti ya Bomet wameachishwa kazi.Kuachishwa kazi kwa wanne hao ilijiri baada ya bodi ya hospitali hiyo, kuwatuma  maafisa hao kwa likizo ya lazima kufuatia kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana kwa umma halkadhalika kwa wahudumu wa hospitali hiyo.

Geofrey Langat amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo kwa muda wa miaka kumi na mitatu, katika hospitali hiyo ambayo inadhaminiwa na kanisa la African Gospel, na kadhalika kupata ufadhili kutoka marekani. Miongoni mwa maafisa walipigwa kalamu ni Raymond Byegon, John Sang na Joseph Maiyo huku hospitali hiyo sasa ikimteua kikaimu Shem Sang’ kushika usukani hadi pale hospitali hiyo itakapopata usimamizi upya wa hospitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *