Wizara ya ardhi humu nchini inaendeleza kampeni ya kusajili mashamba yanayomilikiwa na jamii katika kaunti 25.
Akiongea baada ya kikao na wakazi wa Kapsowar eneo bunge la Marakwet Magharibi kaunti ya Elgeyo Marakwet ,afisa katika wizara hiyo Truphosa Achaa amesema kampeni hiyo inalenga kuwaelimisha wakazi kuhusu kusajili mashamba yanayomilikiwa na jamii.
Afisa huyo aidha ameongeza kuwa kulingana na sheria ya mashamba ya mwaka wa 2016,kuna mashamba katika kaunti 25 yanayomikiliwa ambayo hayajasajiliwa. Aidha afisa huyo amedokeza kuwa hatua hiyo ya usajili itasaidia kusuluhisha mizozo ,na pia kuinuliwa kwa uchumi