Mzee Moi Aaga Dunia

RAIS Mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi, ameaga dunia

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mapema leo Jumanne kwa taifa kufa kwake moi ambapo alifarik  katika hosptali ya Nairobi ambako amekuwa akitibiwa mara kwa mara.Msaidizi wa kibinafsi wa Mzee Moi, Lee Njiru pia amethibitisha kuwa Rais huyo wa pili wa Kenya ameaga dunia.Rais Kenyatta amemtaja Mzee Moi kama kiongozi aliyejitolea kuwakuza na kuwaandaa viongozi wengine si tu nchini Kenya, lakini pia nje ya mipaka ya taifa.

Katika salamu zake za pole, kiongozi wa nchi amefariji wanawe Moi, jamaa pia na marafiki kwa jumla katika kipindi hiki kigumu.Rais Kenyatta ameamuru kuwa Bendera ya Kenya katika maeneo yote ya umma nchini na katika majengo ya balozi za Kenya na mataifa ya kigeni itapeperushwa nusu mlingoti kuanzia leo Februari 4, 2020, hadi jioni siku ya mazishi.Rais Kenyatta anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na kifo cha mzee moi wakati wowote

Mzee Moi amekuwa akilazwa katika Nairobi Hospital tangu mwaka 2019.Alitawala Kenya kwa miaka 24 tangu 1978 hadi 2002.Aliingia mamlakani 1978 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.Licha ya dua zao Moi aliongoza kwa miaka 24, miezi minne na siku nane Alizaliwa  1924- 2020 na ameaga dunia mwendo wa saa  kumi na moja na dakika ishirini

 asubuhi.Mwili wa moi wa  tayari umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya lee funeral huku viongozi wa taifa la Kenya wakitoa rambi rambi zao wakiongozwa na raisuhuru Kenyatta, naibu wake William ruto, kinara wa odm raila odinga  mwiongoni mwa viongozi wengine ambao walimuminia sifa kochokocho rais mstafuu Daniel torotich moi.Mwanawe Gideon moi ambaye ni seneta wa kaunti ya baringo tayari amehutubia taifa  na kuthibitisha kifo cha mzee moi.Jeshi la Kenya litaongoza mazishi ya rais huyo mstaafu moi.Amefariki akiwa na miaka 95.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *