Msongamano Shule ya Kakamega Primary, Wanafunzi Wakiaga Dunia

Zaidi ya wanafunzi 13 walifariki dunia jana jioni katika Shule ya Msingi ya Kakamega shuleni huku  39 wakijeruhiwa.Maafa hayo yalisababishwa na purukushani iliyozuka  wakati wanafunzi hao wakitoka madarasani kuelekea nyumbani.Inasemekana ya kwamba wanafunzi hao Walikanyagana na wengine kuanguka kutoka orofa ya tatu.Baadhi ya wanafunzi wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Kakamega huku wengine 20 walitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.

Kamanda wa Polisi, ukanda wa Magharibi Peris Kimani alithibitisha idadi ya walioaga dunia katika kisa hicho cha kusikitisha nyakati za jioni.Hali imeji wakati ambapo wahudumu wachache tu ndio walikwepo kutokana na mgomo unaoendelea wa madaktari katika kaunti hiyo Kwa hivi sasa shule hiyo imefungwa kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *