Naibu rais William Ruto ametoa wito kwa kanisa kuliombea taifa ili kujikwamua kutoka kwa lindi la maovu ambayo yanatishia kulemaza ukuaji wa taifa hili.
Naibu rais aliwataka viongozi wa kidini kuzidi kukaza kamba katika maombi yao ili amani iweze kudumu katika eneo hili la bonde la ufa swala ambalo lilikuwa likishinikizwa na mwendazake asofu Korir. Naibu rais alikuwa akizungumza hii leo katika hafla ya kusimikwa kwa askofu wa jimbo katoliki la Eldoret askofu Dominic Kimengich hapa mjini, ambapo aliwataka viongozi kujiepusha na visa vya ufisadi ukabili na kuwagawanya wananchi.