Mgomo wa wahudumu wa afya unaingia wiki ya pili leo wakenya wakizidi kuhangaika kupata huduma za matibabu haswa katika hospitali za umma.
Wauguzi wamesisitiza kwamba kamwe hawatarejea kazini hadi pale matakwa yao yote yatakapoangaziwa na serikali hali kadhalika serikali za kaunti.
Magavana nao wametishia kuwatimua wauguzi wanaogoma na wauguzi wanasema maisha yao yamo hatarini haswa wakiwa mstari wa mbele kuwahudumia wagonjwa bila vifaa vya kujiki wakati huu wa ijanga la corona.