wakristo wamehimizwa kutenda mema kwa wenzao kila wakati katika kuimarisha uhusiano wao na mwenyezi mungu.
katika homilia ya moja kwa moja kwenye kanisa la moyo mtakatifu wa yesu hapa kathedrali padre david kiptoo
amesema kuwa wakrsto wanafaa kuwajali wenzao kupitia shukrani wakiwa bado wako hai kama njia ya kumshukuru mwenyezi mungu.
Amewahimiza wakristo watembee pamoja na wenzao katika safari ya duniani kwa kuwasaidia kwa kile watawaweza ili wapate Baraka kutoka kwa mwenyezi mungu.
Amewaeleza umuhimu wa kushirikia pamoja kwa kila jambo kama njia bora ya kujijenga kiimani na pia kutambua uwepo wa mungu kati yao.