Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret askofu Dominich Kimengich, ametoa wito kwa wakristo kumrejelea mwenyezi mungu hasaa katika kipindi hichi na wakati ambapo taifa linayumbishwa kutokana na mkurupuko wa virusi vya corona. Akizungumza na kituo hiki askofu amewahimiza wakristo kila wanapoamka kumrudishia mwenyezi mungu shukrani na pia iwapo wanapata muda basi wapate Ekaristia takatifu
Kuhusu uwezekano wa wakristu wanavyotarajiwa kupata komunyo takatifu askofu amewasihi wale wanaoishi karibu na kanisa kuwa wanaweza kupokea komunyo takatifu nje ya misa huku pia akiwakumbusha wakristu kusalia rosary popote pale wanapojaliwa kupata nafasi ya kusali.
