jimbo katoliki la Eldoret litarajiwa kuandaa kongamano la pili la Ekaristia mwezi Juni mwaka huu katika eneo la Burnt Foresst.
kongamano hili ambalo litahusisha hija na kuabudiwa kwa ekaristia takatifu ni la pili katika jimbo huku wakristu wakitakiwa kushirikiana na wengine kwa sala katika eneo hilo takatifu.
Kongamano la kwanza la Ekaristia liliandaliwa mwaka wa 2022 ambapo lengo kuu lilikuwa na kuombea uchaguzi wa amani askofu Mkuu mwandamizi Dominic Kimengich akiongoza maadhimisho hayo kule Burnt Forest.
