Siku moja baada ya maadhimisho yam isa ya kumbukumbu la wafiadini kule Namugongo nchini Uganda kusitishwa na serikali baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini Uganda limesisitiza kuwa maadhimisho hayo yataendelea.
Baraza hilo chini ya uenyekiti wa askofu Joseph Anthony Zziwa limekariri kuwa wafiadini hao walichangia pakubwa ukuaji wa Imani katika taifa hilo hivyo kumbukumbu ya wafiadini hao iataendelea katika ngazi ya parokia tarehe tatu mwezi juni kwa mwongozo wa askofu wa jimbo.
Hata hivyo maaskofu hao wameridhia ombi kuwa maadhimisho haya hayatukuwepo katika eneo la Namugongo na kutoa wito kwa waumini wote kuwaombea waathiriwa waugonjwa huo wa Ebola Pamoja na wahudumu wa afya wanaowashughulikiwa waathiriwa hao.
Tangazo hili linakuja siku moja baada ya rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhairisha maadhimisho hayo na kuamuru mahujaji waliokuwa wakielekea katika eneo hilo kurejea nyumbani kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Uganda.
