Sakramenti kifungua macho ya mkristu

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Vincent Odundo ametoa wito kwa wakristu kuishi maisha ya sakramenti ambayo anasema itawafungua macho waliopofuka na kuona mwanga wa kristu.

Akihubiri katika parokia ya St.Anthony Of Padua Raliew jimbo kuu katoliki la Kisumu askofu msaidizi alitoa wito kwa kila mmoja kukumbatia sakramenti ya toba mbayo anasema hujenga uhusiano kati ya mja na muumba wake.

Vilevile,askofu huyo alisema kuwa sakramenti hizo huondoa kiburi na majigambo.

Aidha,alisisitiza kuwa uwepo wa roho mtakatifu umwongoza mkristu katika maisha matakatifu na uzima wa milele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *