Watu wawili waliteketezwa hadi kufa na wananchi wenye ghadhabu baada yao kudaiwa kuhusika na wizi wa simu katika mtaa wa Munyaka viungani mwa jiji la Eldoret usiku wa kuamkia jumatano.
Yaaminika kuwa, wawili hao walikua wamemwibia mpita njia simu ambaye alipiga kamsa ambao uliwavutia wananchi na ambao waliwashambulia na kuwapa kichapo cha mbwa kabla ya kuteketezwa hadi wakafariki.
Akithibitisha haya kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi alisema kwamba miili ya wawili hao ilihamishiwa katika hifadhi ya hospitali ya mtrh Eldoret
Mwanthi aliwataka wananchi kutochukua sheria mkononi na badala yake kupasha maafisa wa polisi habari pindi wanamkamata mhalifu yeyote ili waweze kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.