Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Peter Makau ameitaka serikali ya kitaifa kuangazia kiukamilifu usalama wa wananchi katika kaunt hiyo nae neo pana la Kaskazini mashariki mwa nchi kunakosuhudiwa uvamizi vya mara kwa mara.
Kulingana naye,mashamubilizi ya hivi karibuni yayowaacha watu wawili wamefariki kufuatia shambulio ya watu wanaoaminika kuwa magaidi wa Al-Shabaab,imewafanya wananchi kuishi kwa hofu swala ambalo lastahili kushughulikiwa mara moja.
Alisema kwamba wakazi kwa sasa wanashindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku akiongeza kuwa huenda hili likapelekea kudorora kwa Uchumi wa eneo hilo.
Yanajiri haya wakati na ambapo,Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen akiwalaumu baadhi ya maafisa wa usalama eneo hilo wanaoaminika kufunga shughuli za kupiga doria mapema wakiwaacha wananchi mikononi mwa magaidi,huku akiahidi kuanza upya kwa shughuli ya utwaliwaji wa silaha haramu kwa wananchi ili kuimarisha amani.
