Ulimwengu ukisherekea siku ya ugonjwa wa saratani,imebainika kuwa watu zaidi ya elfu Hamsini hupoteza maisha yao kutokana na saratani aina tofauti tofauti nchini.
Akiongea katika hospitali ya Moi MTRH wakati wa maadhimisho haya,afisa msimamizi wa maafisa wanakliniki katika hospitali ya MTRH Dkt.Andrew Wandera alisema visa vya ugonjwa huo unachangiwa sana sana na watu kukosa kujitokeza na kujua hali yao ya kiafya kwa wakati mwafaka.
Aliongeza kuwa,hospitali ya Moi ni mojawapo ya hospitali kuu nchini ambazo zinategemewa kwa matibabu ya saratani na wanaendelea kushirikiana na washikadau mbalimbali kupanua shughuli za matibabu kwenye kitengo hicho.
Kwa upande wake,afisa mkuu wa Idara ya afya anayehusika na kudhibiti magonjwa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Paul Wangwe amesisitiza haja ya wananchi kuhamasishwa vya kutosha kuhusu umuhimu wa kujipima ili iwapo wanaishi na Saratani waweze kupata matibabu mapema na kupunguza mzigo wa gharama ya matibabu baaday.
Aliongeza pia kuwa,kaunti ya Uasin Gishu ina vituo mia moja na arobaini na tatu kote kaunti na wahudumu wa afya nyanjani CHPs wapatao elfu mbili na tano kwenye vituo mbalimbali.
