Meneja wa bodi ya kitaifa na nafaka na mazao (NCPB) kaunti ya Uasin Gishu Gilbert Rotich, amewahakikishia wakulima kuwa kuna mbolea ya kutosha katika bodi hiyo wakati huu wanapojiandaa kwa upanzi.
Katika mahojiano ya kipekee na idhaa hii afisini mwake, Rotich amewaondolea hofu wakulima kuhusu uhaba wa mbolea ya ruzuku akiwataka kutembelea maghala ya bodi hiyo ili kupata bidhaa hiyo.
Wakati uo huo meneja huyo amesifia mikakati ambayo serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na zile za kaunti imeweka ili kurahisisha upatikanaji wa mbolea ya bei nafuu.
Kwa upande wake mkulima mmoja kutoka kaunti ya Uasin Gishu ameeleezea kuridhishwa na huduma ya usambazaji wa mbolea wakulima hasa wakti huu wanapojiandaa kwa smimu wa upanzi.
