Azimio ya kulinda Amani Jimbo la Darfur

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litapitisha azimio jipya litakalobadili mamlaka ya ujumbe wa kulinda amani jimboni Darfur nchini Sudan, na kuanzisha ujumbe wa kisiasa na amani.

Jukumu lake kuu litakuwa kuisaidia Sudan katika kipindi cha mpito kuelekea demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba mpya na uchaguzi.

Rasimu ya azimio hilo kimsing itaondoa ujumbe mkuu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, maarufu UNAMID, na majukumu yake kukabidhiwa kwa serikali ya mpito ya Sudan.

Ujumbe mpya utakaoundwa chini ya azimio hilo utajulikana “Ujumbe wa kisiasa na kujenga amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan – UNPPIMS. Azimio hilo linafuata kwa sehemu kubwa mapendekezo yaliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, na mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Faki Musa Faki, katika ripoti yako iliyowasilishwa kwa Baraza kuhusu hali jimoni Darfur.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *