Mudavadi; Serikali inastahili kuweka mikakati ya kukinga Uchumi kutokana na athari za Corona

Kinara wa chama cha Amani National Congress ANC Musalia Mudavadi ameitaka serikali kuweka mikakati kabambe ya kuhakikisha inawakinga wakenya kutokana na athari za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.

Mudavadi amesema huenda uchumi wa taifa ukazorota hata zaidi huku akionya kwamba huenda wakenya wengi wakapoteza ajira kutokana na hali hiyo. Amesema serikali ya kitaifa pamoja na zile za kaunti zinafaa kulegeza masharti yao kuhusu utoaji ushuru wakati huu na kuonya kampuni zinazotoa huduma dhidi ya kuwakatizia wakenya huduma kama vile umeme na maji wakati huu wa janga la Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *