Wakristu wametakiwa kufanya mabadilko katika maeneo yao ya kazi kwa kuonyesha wale wanaotangamana nao katika sehemu hizo ukarimu.
Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima akihubiri katika warsha ya walimu wakuu wa shule zinazomilikiwa na kanisa katoliki nchini askofu kadima amesema kuwa njia bora ya kuboresha maeneo ya kazi ni kuwa wakarimu na siku zote kuwa na hulka ya kushukuru katika kila jambo.
Amewahimiza kila mfanyikazi kutangamana na wale wanaofanya nao kazi kwa upendo akisema kuwa upendo huo huweka hai matumaini yaw engine kuurithi ufakme wa mbingu.
