Pope; LGBTQ haina nafasi ya ukuhani kanisani

Baba mtakatifu Francisko amewatahadharisha wale wanaoshiriki mahusiano ya jinsia moja almaarufu LGBTQ akisema kuwa kanisa kamwe halitavumilia hulka hiyo.

Akihutubu katika mkutano moja wa faragha mjini Vatican na makasisi, Baba mtakatifu amesema kuwa wale wanaoshiriki mahusiano hayo hawatapewa nafasi ya kuwa mapadre au watawa katika kanisa, jambo ambalo anasema linakinzana na mafundisho ya Bibilia.

Tuhuma hizi mpya zinaripotiwa ikiwa ni wiki chache baada ya wale wanaoshiriki mahusiano hayo, kutaka Baba Mtakatifu kuomba radhi kwa kuwakanya dhidi ya hulka hiyo wakidai kuwa papa aliwabagua. Ikijibu tuhuma hizi mpya, Ofisi ya Habari ya Vatikan imekariri taarifa waliyoitoa awali kuhusu mkutano huo wa Jumanne baina ya Papa na Makasisi, ambapo mkuu huyo wa Kanisa Katoliki alikariri hitaji la kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja Kanisani, na haja ya tahadhari kuhusu wao kuwa makasisi akisisitiza kuwa kamwe hawana nafasi ya kuwa makasisi katika kanisa katoliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *