Baba mtakatifu Francisko ametoa wito kwa wachekeshaji duniani kukoma kukejeli makanisa bali wawe chombo bora cha uinjilishaji .
Katika mkutano uliowaleta pamoja wachekeshaji mia moja na saba kutoka katika mataifa kumi na tano duniani, baba mtakatifu amewapongeza kwa juhudi zao za kuunganisha na kuleta watu pamoja kupitia vichekesho, akiwahimiza kuendelea siku zote kuleta furaha nyusoni mwa watu.
Hata hivyo baba mtakatifu Francisko amewatahadharisha dhidi ya kufanya maigizo yanayodhihaki na kukosea heshima kanisa, akisema kuwa kanisa ni sehemu mahalia ya Mungu nyumba ya wote na kule kukejeli kanisa ni sawia na kumkosea heshima mwenyezi Mungu.