Viongozi Nandi wataka majadiliano katia VAT

Viongozi wa Kidini katika kaunti ya Nandi wamewataka wabunge kuwa makini kabla ya kupitisha mswada tata wa kifedha wa 2024 ili isije ikamkandamiza mkenya wa kawaida.

Wakiongozwa na askofu wa kiangilikana dyosisi ya Kapsabet Paul Korir,viongozi hao wanasema mswada huo unapaswa kupigwa msasa ipasavyo,kabla ya kuupitisha ndipo isije ikamvurutia chini mkenya wa kawaida.

Waakizungumza mjini Kapsabet,viongozi hao wametoa pendekezo kwa wabunge kufanyia marekebisho kwanza mswada huo kabla ya kupitisha kuwa sheria,kwani wanasema wakenya wanapitia hali ngumu ya maisha na pana haja ya kurekebishwa.

Wamewataka viongozi kupunguza cheche za maneno ambayo huenda ikachochea uhasama miongoni mwa wakenya,na kusaidia taifa kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *