Muungano wa wafanyikazi COTU tawi la kaunti ya Uasin Gishu imelaani vikali kisa cha kuvamiwa na kuuawa kwa hakimu katika mahakama ya Makadara kwa kupigwa risasi na mume wa mshukiwa mmoja.
Akizungumza mjini Eldoret,katibu wa chama hicho Peter Odima alisema kwamba serikali inapaswa kuimarisha usalama katika Mahakama za humu nchini maana ndio mahali ambapo wakenya wanapata haki,na kukikosekana usalama wakenya huenda wakashindwa kutafuta haki kwenye mahakama za humu nchini.
Yanajiri haya baada ya Hakimu mwandamizi wa Mahakama ya Makadara monica Kivuti alipigwa risasi kifuani Alhamisi alasiri na mguuni na afisa wa polisi baada ya kutoa uamuzi kuhusu kesi iliyomhusisha mke wa afisa huyo wa polisi.