Waziri anayesimamia elimu katika kaunti ya Elgeyo marakwet Edwin kibor ametoa wito kwa wazazi na washikadau wote wa elimu katika kaunti hiyo kushirikiana Kwa pamoja kama njia moja ya kuboresha elimu.
Haya kutokana na matokeo duni ambapo wanafunzi 81 walipata alama ya E katika mtihani wa kitaifa wa mwaka uliopita WA KCSE katika eneo bunge la keiyo kazkazini.
Maongezi yake Kibor yaliungwa mkono na mwakilishi wadi ya Emsoo Christopher cheboiboch, ambaye pia ni mwenyekiti wa Elimu katika bunge la kauti ya Elgeyo marakwet, ambaye ametaka wanafunzi kuwa na nidhamu Ili waweze kufaulu shuleni.
Cheboiboch aidha alisitiza kuwa wao kama viongozi wataendelea kushirikiana ili kukabiliana na changamoto kadhaa ikiwa pamoja na kufanikisha ujenzi wa madarasa pamoja na kusaidia wanafunzi wasiojiweza, kupata karo na kuendelea na masomo yao.