Sakramenti ngao ya maisha

Waumini wametakiwa siku zote kuwa mashuhuda wakristu kwa kutilia maanani sakramenti na hatimaye kuishi maisha hayo.

Haya ni kwa mujibu wa askofu wa jimbo katoliki la Garissa George Muthaka ambaye alitoa wito kwa kila mkristu kujisadaka na kuwa miongoni mwa mashuhuda wakristu watakaosambaza habari njema ya kristu kwa watu wote wanaoishi katika dunia hii iliyojaa kelele mingi.

Askofu huyo kadhalika alitoa wito kwa waumini kusimama kidete katika imani hiyo ambayo anasema kuwa ndio msingi wa kristu na kamwe wasipoteze matumanini katika kristu.

Alisema kuwa namna ya kuweka hai matumaini kwa wale waliovunjika moyo ni kuwaonyesha mfano bora wa maisha ya sakramenti akibaini kuwa sakramenti hizo ndizo humpa mkristu hekima ya kutenda yale yaliyo mema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *